Zimebaki dakika 3 kumaliza sura

Yaliyomo

Nguzo Iliyosahaulika

Sura 9 · 3 dakika za kusoma

Suluhisho sahihi

Mungu amempa Dada White mawasilisho kuhusu udanganyifu ambao Shetani analeta ndani ya kanisa letu. Aliagizwa kwamba tunapaswa kusoma na kuelewa maneno ya mapainia ili kupambana na udanganyifu huu.

Ellen G. White:

Nimekuwa na mawasilisho kuhusu udanganyifu ambao Shetani analeta ndani katika wakati huu. Nimeagizwa kwamba tunapaswa kuweka kipaumbele ushuhuda wa baadhi ya wafanyakazi wa zamani ambao sasa wamekufa. Waache waendelee kuongea kupitia kwa makala yao kama inavyopatikana katika nambari za mapema za majarida yetu. Nakala hizi sasa zinapaswa kuchapishwa tena, ili kuwe na sauti iliyo hai kutoka kwa mashahidi wa Bwana. Historia ya uzoefu wa mapema katika ujumbe utakuwa nguvu ya kuhimili ujanja mkuu wa Udanganyifu wa Shetani. Agizo hili limerudiwa hivi karibuni. Lazima niwasilishe mbele ya watu ushuhuda wa ukweli wa Biblia na kurudia jumbe zilizoamuliwa zilizotolewa kwa miaka iliyopita...

Lt99-1905.7; 1905
Ellen G. White:

Wanadamu wanapoingia ambao wangehamisha nguzo moja au nguzo kutoka kwenye msingi ambao Mungu ameimarisha kupitia kwa Roho wake Mtakatifu, waache wazee waliokuwa waanzilishi katika kazi yetu waongee waziwazi, na wacha wale waliokufa waongee pia kwa kuchapishwa kwa makala yao tena ndani ya magazeti yetu. Kusanya miale ya mionzi ya kimungu ambayo Mungu ametupea kama alivyowaongoza watu wake hatua kwa hatua katika njia ya ukweli. Ukweli huu utastahimili mtihani wa wakati na kesi.

Ms62-1905.20, 1905

Tumeona kwamba Kanisa la Waadventista Wasabato limepata mabadiliko katika misingi yetu kuhusu Umbile la Mungu. Tumeambiwa kwamba ukweli wa kwanza uliopokelewa na waanzilishi wetu utastahimili mtihani wa wakati na jaribio. Je, ukweli juu ya Umbile la Mungu, ambao tumepokea kwanza, umeanguka mtihani wa wakati?

Ellen G. White:

Nguvu ya Mungu inaposhuhudia kile ambacho ni kweli, ukweli unafaa kusimama milele kama ukweli. Hapana dhana ya kuchipuka baadaye, kinyume na mwanga ambao Mungu amepeana inapaswa kupewa nafasi au ruhusa. Watu watainuka wakiwa na tafsiri za Maandiko ambazo kwao ni kweli, lakini si ukweli. Ukweli wa wakati huu, Mungu ametupa kama msingi wa imani yetu. Yeye Mwenyewe ametufundisha ambacho ni ukweli. Mmoja atatokea na mwingine pia na mwanga mpya ambao unakinzana na nuru ambayo Mungu amepeana chini ya onyesho la Roho wake Mtakatifu. Wachache bado wako hai ambao walipitia uzoefu uliopatikana katika kuanzishwa kwa ukweli huu. Mungu kwa neema ameyaokoa maisha yao kurudia na kurudia hadi mwisho wa maisha yao, uzoefu ambao walioipitia hata kama alivyopitia Yohana mtume hadi mwisho kabisa wa maisha yake. Na washikaji viwango walioanguka katika mauti, wanafaa kunena kupitia kwa njia ya uchapishaji upya wa maandishi yao. Nimeagizwa kwamba sauti [zao] zisikike. Wanapaswa kutoa ushuhuda wao kuhusu kile kinachojumuisha ukweli wa wakati huu. Hatufai kupokea maneno ya wale wanaokuja na ujumbe unaopingana na pointi maalum za imani yetu. Wanakusanya Maandiko mengi, na kuyarundika kama uthibitisho kuzunguka nadharia zao wanazodai. Hii imefanywa tena na tena katika kipindi cha miaka hamsini iliyopita. Na maadamu Maandiko ni Neno la Mungu, na yanapaswa kuheshimiwa, matumizi ya yao, ikiwa matumizi hayo yatasongesha nguzo moja ya msingi ambao Mungu ameendeleza miaka hii hamsini, ni kosa kubwa. Yeye ambaye hufanya matumizi kama hayo hajui onyesho la ajabu la Roho Mtakatifu aliyeipea nguvu jumbe zilizopita ambazo zimewafikia watu wa Mungu.

PH020 14.2; 1905

Hebu tufahamiane na uandishi wa waanzilishi wetu kuhusu hoja ya kwanza ya Kanuni za Msingi. Hebu tufahamiane na ukweli ambao mapainia waliandika kuhusu Umbile la Mungu na mahali uwepo wake ulipo. Hebu, tukusanye miale ya nuru ya kimungu ambayo Mungu amewapea kama alivyowaongoza watu wake hatua kwa hatua katika njia ya ukweli.1

Now heed the words of those long past,
Their sacred truths were built to last.
Return to pillars set with care,
For God revealed His nature there.

Deceptive errors have crept in,
To move the pillars is a sin.
The pio'neers’ voices still should speak,
Their ancient wisdom we should seek.

For Ellen counseled in her day,
From early light we must not stray.
God’s personality divine,
This truth the pioneer words define.

Tanbihi

  1. 1